Featured
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo MICHEZO. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo MICHEZO. Onyesha machapisho yote

Jumatatu, 2 Mei 2016

Jedwali la msimamo wa ligi ya EPL

Jedwali la msimamo wa ligi ya EPL kufikia 2 Mei, 2016.
NambariKlabuMechiMabaoAlama
1Leicester363077
2Tottenham353969
3Arsenal362567
4Man City363064
5Man Utd351260
6West Ham351759
7Southampton361457
8Liverpool351155
9Stoke36-1448
10Chelsea34747
11Everton35644
12Watford35-644
13Swansea36-1343
14West Brom36-1441
15Bournemouth36-2041
16Crystal Palace36-1039
17Newcastle36-2533
18Sunderland35-1832
19Norwich35-2631
20Aston Villa36-4516

Leicester City kunyemelea ushindi Epl?

Image copyrightbbc
Image captionLeicester City imetoka sare ya 1-1 ilipokutana na Manchester United
Leicester City wamebakiwa na alama mbili pekee kuupata ushindi wa ligi kuu ya England baada ya kupata sare ya 1-1 dhidi ya klabu ya Manchester United katika dimba la Old Trafford huku wakitegemea matokeo ya mchezo kati ya Chelsea dhidi ya Tottenham utakaopigwa leo hii majira ya saa nne usiku kwa saa za afrika mashariki katika dimba la Stamford Bridge.
Mbweha walipata afueni baada ya kuwa nyuma kwa goli moja lililofungwa na Antony Martial dakika ya nane ya mchezo kabla ya kusawazisha na kepten Wes Morgan dakika ya 17. Pande zote mbili zilinyimwa mikwaju ya penalti baada ya mlinzi Marcos Rojo kumzuia Riyad Mahrez ndani ya eneo la 18 huku pia Danny Drinkwater wa Leicester akimvuta Memphis Depay ndani ya eneo la hatari.
kwa matokeo hayo Leicester wanaendelea kubaki kileleni mwa ligi ya England wakiwa na alama 77. Claudio Ranieri huyo akisisitiza kuwa hawakufuata kikombe OT bali kucheza mchezo safi lakini Man U walikua wazuri zaidi yao. Matokeo mengine Liverpool walikiona cha mtema kuni baada ya kuchapwa 3-1 walipokuwa wageni wa Swansea huku Man city wakiambulia kichapo cha mbwa mwizi 4-2 walipowatembelea Sauthampton

Wenger: Nilitarajia mabango zaidi Emirates

WengerImage copyrightAFP
Image captionWenger anasema mashabiki wana haki ya kulalamika
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema alitarajia mashabiki zaidi waonyeshe kutoridhishwa naye wakati wa mechi ya Jumamosi dhidi ya Norwich.
Arsenal walishinda 1-0.
Wenger atatimiza 20 kwenye usukani Arsenal Oktoba mwaka huu lakini mara yake ya mwisho kushinda ligi ilikuwa 2004 na baadhi ya mashabiki waliinua mabako ya kusema “wakati wa mabadiliko umefika” uwanjani Emirates.
"Nilidhani uwanja wote ungegeuka na kuwa wa rangi nyeupe (kutokana na mabango),” amesema.
"Lengo letu kuu ni kuwafanya watu wote 100% wafurahi. Kwa bahati mbaya, hatukuweza kufanya hilo msimu huu.”
Ushindi wa Jumamosi uliwawezesha Arsenal kuwapita Manchester City, ambao watakuwa wenyeji wa The Gunners uwanjani Etihad Jumamosi, na kutua nambari tatu jedwali la Ligi ya Premia.
Arsenal wanahitaji alama mbili kutoka kwa mechi zao zilizosalia kujihakikishia nafari katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu ujao, kwa mara ya 18 mtawalia.
ArsenalImage copyrightAll Sport
Image captionBaadhi ya mashabiki hawajafurahia kushindwa kwa Arsenal kushinda ligi
Wakati wa mechi hiyo ya Norwich, baadhi ya mashabiki walinyanyua mabango dakika za 12 na 78 za mechi, kuachilia miaka 12 tangu Arsenal walipotawazwa mabingwa ligi mara ya mwisho.
Lakini kunao wengine walioeleza uungaji mkono wao kwa Wenger.
"Mimi ni mtu wa soka. Mimi si mwanasiasa,” alisema Wenger, 66.
"Simo katika mfumo wa demkrasia. Nitakuwepo mechi ijayo, kusimamia mechi, kujaribu kufanya vyema na nakubali maoni ya watu,” alisema.
Mkataba wa Wenger utamalizika msimu wa 2016/17 na anasema hapangi kung’atuka kabla ya wakati huo.

Vardy mchezaji bora wa mwaka Uingereza

VardyImage copyrightAP
Image captionVardy amefunga mabao 22 ligini msimu huu
Mshambuliaji wa Leicester Jamie Vardy ametawazwa mchezaji soka bora wa mwaka na chama cha waandishi wa kandanda Uingereza.
Mshambuliaji huyo wa Uingereza alipata 36% ya kura zilizopigwa na wanahabari 290 na kuwashinda wenzake Riyad Mahrez na N'Golo Kante.
Vardy, 29, amefunga mabao 22 Ligi ya Premia msimu huu.
Aidha, alivunja rekodi kwa kufunga mabao kila mechi katika mechi 11 mtawalia.
Klabu yake inahitaji alama mbili pekee kushinda Ligi Kuu ya Uingereza lakini inaweza pia kutawazwa mabingwa iwapo Tottenham watashindwa kuwalaza Chelsea jioni.
Mahrez alishinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka ya PFA, ambayo mshindi hupigiwa kura na wachezaji soka ya kulipwa, mwezi jana.

Ranieri kutotazama mechi muhimu ya Spurs

Ranieri
Image captionRanieri atakuwa akirejea Uingereza kutoka Italia
Meneja wa Leicester Claudio Ranieri amesema huenda akashindwa kutazama mechi muhimu ya leo jioni kati ya Chelsea na Tottenham.
Iwapo Tottenham watashindwa kuondoka na ushindi uwanjani Stamford Bridge, basi Leicester watatawazwa mabingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza msimu wa 2015/16.
"Ningependa sana kutazama mechi hiyo ya Tottenham lakini nitakuwa kwenye ndege nikisafiri kutoka Italia,” Ranieri amesema.
"Mamangu anatimiza umri wa miaka 96 na ningependa sana kula naye chakula cha mchana. Nitakuwa mtu wa mwisho Uingereza kufahamu (matokeo).”
Mwitaliano huyo hajawahi kushinda ligi kuu katika maisha yake ya ukufunzi lakini sasa Leicester wanahitaji alama mbili pekee kutawazwa mabingwa baada yao kutoka sare 1-1 na Manchester United Jumapili.
Ranieri hata hivyo amesema anatarajia Spurs, waliosalia na mechi tatu, waongeze muda wao wa kusubiri kushinda taji.
Iwapo Spurs watashinda leo basi Leicester wanaweza kutawazwa mabingwa wakifanikiwa kulaza Everton Jumamosi.
"Akilini mwangu, Tottenham watashinda mechi zao zote tatu," alisema. "Naangazia sana mechi dhidi ya Everton."
Copyright © 2015 TANZANIA YETU
| Distributed By Gooyaabi Templates